Wito kwa mafunzo ya muziki, Ethiopia

Wito kwa wanamuziki wa Kitanzania kushiriki katika mafunzo ya muziki itakayofanyika mwezi Julai 2020 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Wanamuziki wa kike wanahimizwa kuomba!

Shule ya Muziki ya Jazzamba kwa kushirikiana na Goethe-Institut Addis Ababa inaandaa semina ya mafunzo ya Siku 20 huko Addis Ababa, Ethiopia. Kwa Tanzania, zoezi la kuchagua washiriki hao linasimamiwa na Action Music Tanzania na Global Music Academy ambao wanatafuta timu ya wanamuziki tisa kutoka Tanzania, ili kuhudhuria programu hiyo ya mafunzo.

Tunawatafuta wanamuziki wanaocheza, Kinanda, Gitaa, Gitaa la umeme la bass, Saxophone, Trombone, Lipi (Trumpet), Drums, wapiga ngoma na waimbaji. Ikiwa unapiga moja ya vyombo hivi, hii inaweza kuwa nafasi uliyokuwa ukiitafuta.

Waombaji watakaochaguliwa wataalikwa kushiriki katika semina ya maandalizi itakayofanyika Action Music Academy, jijini Dar es Salaam mwezi Machi 2020. Ambapo Wanamuziki tisa watachaguliwa kwenda kushiriki katika Kampasi ya Muziki (East African Creative Music Campus) ambayo itafanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Julai 2020 na mwezi Juni 2021. Kampasi hiyo inafadhiliwa na Goethe-Institut na mpango wa Erasmus + wa Jumuiya ya Ulaya.

Je ungependa kushiriki mafunzo haya? Ikiwa una nia ya kushiriki tafadhali jaza fomu ya maombi na tutawasiliana nawe juu ya uteuzi wako. Ikiwa una maswali yoyote zaidi wasiliana na Action Music Academy Tanzania kwa barua pepe kwa [email protected]

Unaweza kupata fomu ya kushiriki hapa

Kwa habari zaidi tembelea: www.global-music-campus.net

Download this post as a PDF document.

AMTZ would like to thank the following partners for their generous support.

Sponsor logos