Mafunzo Ya Muziki Kwa Vijana, Wanakwaya Na Walimu Wa Muziki

Vijana, wanakwaya na walimu wa muziki wanaalikwa kujiunga na mafunzo ya muziki kwenye chuo cha Action Music Academy (AMA), kilichopo Mbezi Beach Goigi mkabala na shule ya St Mary’s Junior International Academy, Jijini Dar es Salaam. Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala mbalimbali za muziki kupitia kozi za muda mfupi na mrefu (miezi mitatu na mwaka mmoja).

Kumekuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki makanisani jambo linalochangia wanamuziki wengi kujenga kasumba ya kuhamahama kutoka kanisa moja kwenda jingine na hivyo kuyumbisha maendeleo ya uinjilishaji kwa njia ya muziki katika kanisa husika baada ya wao kuondoka.

Action Music Tanzania (AMTZ) kupitia AMA imeanzisha mafunzo ya Muziki kwa lengo la kuwaandaa wanamuziki kuwa na uwezo wa kuandaa, kucheza na kufundisha muziki kwa kutumia mbinu mpya na za kitaalamu ili kuambukiza elimu ya muziki kwa wanamuziki wengine na hatimaye kuboresha ustawi wa muziki wa makanisani.

Masomo yanayofundishwa yanamuandaa mwanafunzi kujipatia ajira katika tasnia ya muziki sio tu kama mwanamuziki mtaalamu ila pia kama mwalimu wa muziki na recording engineer.

AMA inaomba ushirikiano wako katika kufanikisha mafunzo haya kwa kuwapa hamasa vijana wa kanisa lako kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika mafunzo hayo. Gharama za mafunzo ni shilingi 120,000 kwa mwezi kwa muda wa miezi tisa.

Action Music Tanzania (AMTZ) ni asasi isiyo ya kiserikali inayoundwa na walimu wa muziki kutoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya muziki nchini na imesajiliwa na BASATA (No. BST/4733) na kupata kibali cha kutoa mafunzo ya muziki ya muda mfupi.

Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Action Music Tanzania (AMTZ)

AMTZ would like to thank the following partners for their generous support.

Sponsor logos